Zahran Mamdani, Mbunge wa jimbo na mgombea wa chama cha Demokratik katika uchaguzi wa Umeya wa New York, kupitia kampeni za wananchi amefanikiwa kuwashinda wapinzani maarufu kama Andrew Cuomo katika kinyang’anyiro cha awali na kuwa mgombea wa kwanza Mwislamu kwa nafasi hiyo. Ushindi huo, hata hivyo, umekumbwa na mashambulizi ya chuki na matusi ya Uislamu kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, lakini yeye pamoja na wafuasi wake wametangaza kuwa hawatarudi nyuma mbele ya chuki na ubaguzi.