Wachezaji na viongozi wa msafara wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran wamefanya majlisi ya maombolezo ya Tasu'a ya Imam Hussein (a.s.) katika makazi yao mjini Tijuana, Mexico, wakikumbuka mashahidi wa Karbala na kuonyesha mapenzi yao kwa Ahlul-Bayt (a.s.).
Machafuko nchini Mexico yanaendelea kufuatia kifo cha kiongozi wa moja ya karteli hatari, huku wanajeshi 25 wa Walinzi wa Taifa wakiripotiwa kuuawa katika wimbi la vurugu.
Maelfu ya wananchi mjini Mexico City waliungana katika maandamano makubwa yaliyopewa jina “Mexico kwa Palestina”, wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani, huku wakidai kusitishwa kwa mauaji ya kimbari Gaza na kutumwa haraka kwa misaada ya kibinadamu.