Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amewasili mjini Muscat, Oman, kwa ziara ya kidiplomasia inayolenga kujadili usimamizi wa Mlango wa Hormuz, maendeleo ya kikanda na kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Oman.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameongozana na ujumbe wake wa kidiplomasia kuelekea mjini Muscat, Oman, kwa ajili ya mazungumzo na Marekani. Mazungumzo hayo yanatazamwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kujadili masuala ya nyuklia, vikwazo vya kiuchumi na usalama wa kikanda, kwa lengo la kufungua ukurasa mpya wa maelewano ya kisiasa.