Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, ameonya kwamba kundi la mapambano lina haki ya kulipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa kamanda mwandamizi Haitham Al-Tabtabai, na akasisitiza kuwa kujisalimisha si chaguo kabisa.
Sheikh Ali Damuush amesema: “Kulegeza msimamo au kukubali mashinikizo na maagizo ya Marekani na Israel hakutaleta matokeo yoyote. Sisi hatutasalimu amri; hata ikiwa maadui wataweka juhudi zao zote kutuangamiza, kamwe hatutaacha njia ya muqawama (mapambano) wala kujitoa katika kuilinda nchi yetu.”