Familia katika mtazamo wa Mtume Mtukufu (s.a.w) si tu kitovu cha utulivu, bali ni uwanja wa kudhihirika kwa maadili ya kimungu. Yeye (s.a.w.w), kwa tabia yake tukufu na kwa kushikamana na mafundisho ya Qur'an kama vile: " - Semeni naye - kwa upole" (قَوْلًا لَّیِّنًا), na "Hakika wewe ni mwenye tabia njema kabisa" (إِنَّکَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِیمٍ), alionesha ustadi wa kipekee katika kuonyesha mapenzi kwa wake na watoto wake.
Makala hii, ikitegemea vyanzo vya Kishia, inachunguza mwonekano wa upendo wa Mtume (s.a.w.w) ndani ya familia, na inatoa mafunzo ya kudumu kwa familia za leo.