Katika mwendelezo wa matamko yanayofichua malengo ya kweli ya utawala wa Kizayuni wa Israel, mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Hamas, Osama Hamdan, amesisitiza kuwa mazungumzo kuhusu kukabidhi silaha za Muqawama hayana msingi wowote. Ameeleza kuwa wakati Israel inakiuka ahadi zake zote, lengo lake kuu linaendelea kuwa ni kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.