Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amekosoa ukimya wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, kuhusu mashambulizi na vitisho vya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, akisema mashambulizi hayo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kanuni za IAEA.
Wizara ya Ulinzi ya Israel imetiliana saini mkataba mkubwa na Kampuni ya Rafael ili kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa makombora ya kukinga ya mfumo wa Iron Dome (Gombo la Chuma).