Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema: Iran na Uturuki si tu nchi jirani, bali ni nchi mbili rafiki na ndugu zenye ushirikiano mkubwa sana.
Katika Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran, vitabu vitatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kazakhi vitazinduliwa rasmi, na miongoni mwao ni kitabu kiitwacho "Rafiki Yetu Mwenye Bahati", ambacho ni wasifu wa Shahidi Jenerali Qasem Soleimani.