Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema Kituo cha Nyuklia cha Bushehr kimeingia miongoni mwa vituo 10 bora vya nyuklia duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo baada ya kupata alama kamili ya 100/100 katika tathmini za kimataifa za usalama na ufanisi wa uendeshaji.
Rais wa Shirika la Nishati ya Atomiki ya Iran katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Mionzi kaskazini-magharibi mwa nchi, alieleza kwamba teknolojia ya nyuklia ni tasnia ya kisasa, na matumizi ya mionzi ni hatua muhimu katika kuboresha afya na usalama wa chakula nchini. Pia alisisitiza kuwa teknolojia hii inaweza kuleta baraka nyingi kwa wananchi wa Iran.