Taabu

  • Tone kutoka Nahj al-Balagha (47): Mcha Mungu Hatoki Katika Njia ya Haki

    Tone kutoka Nahj al-Balagha (47): Mcha Mungu Hatoki Katika Njia ya Haki

    "Nafsi yake iko katika taabu kutokana na yeye mwenyewe, na watu wako katika amani kutokana naye." «نَفْسُهُ مِنْهُ فِی عَنَاءٍ» Nafsi yake iko katika uchungu na taabu kwa sababu ya kujidhibiti kwake mwenyewe. «وَ النَّاسُ مِنْهُ فِی رَاحَةٍ» Na watu wako katika raha na utulivu kutokana naye. «أَتْعَبَ نَفْسَهُ لِآخِرَتِهِ» Ameitia nafsi yake katika juhudi na shida kwa ajili ya Akhera yake. «وَ أَرَاحَ النَّاسَ مِنْ نَفْسِهِ» Lakini amewaweka wengine katika amani kutokana na nafsi yake, kiasi kwamba hawapati madhara wala usumbufu wowote kutoka kwake.