Katibu Mkuu wa Hezbollah amesema kuwa mpango wa kuangamiza Iran na muqawama umefeli, akisisitiza kuwa kusitishwa kwa mapigano lazima kuwe kwa masharti ya kusitishwa kabisa kwa uvamizi na kujiondoa kwa adui katika maeneo wanayoyakalia.
Serikali ya Uingereza hivi karibuni imeweka taratibu kali zaidi za kuchunguza uhalali wa wakurugenzi wa makampuni, imeweka vikwazo dhidi ya viongozi wa RSF, na imerudia wito wake wa kusitishwa mara moja kwa uhalifu, kulindwa kwa raia, na kuhakikisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan.