Mkuu wa Mahusiano ya Kigeni na Mjumbe wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi umoja wa Kiislamu na kufuata mafundisho ya Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) kuhusu huruma na uongofu, akieleza juu ya juhudi endelevu za maadui katika kuharibu sura ya Uislamu.
Historia inaonyesha kuwa jukwaa hili lina mizizi imara katika imani, haki na uadilifu. Lilianza na mtu mmoja au wawili zaidi ya karne kumi zilizopita. Pamoja na changamoto nyingi zilizowakumba waliolipanda, idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila mwaka - hasa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.