Lengo la Mazungumzo Haya ni: Kuleta maelewano baina ya Madhehebu za Kiislamu na kuonyesha kuwa msingi wa Uimamu na Ukhalifa wa Maimam Kumi na Wawili wa Ahlul-Bayt (a.s), wanaofuatwa na Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, una mizizi pia katika vyanzo vinavyokubalika vya Kisunni.
Licha ya kwamba Ahlul-Bayti wa Mtume (s.a.w.w) walikabiliwa na changamoto tofauti kisiasa na kijamii, lakini walijitahidi kuhakikisha wanainua bendera ya dini ya Kiislamu katika zama zao zote. Dakta Shahid Mutwahhari, mwanafikra mashuhuri wa Iran anaandika kwa kusema: " Ahlul-Bayti (a.s) walikuwa wakichunga maslahi ya Kiislamu na Waislamu kwa ujumla".