Utukufu

  • Binadamu Katika Mtazamo wa Qur’an

    Binadamu Katika Mtazamo wa Qur’an

    Qur’ani katika asili ya kila binadamu, hata kama ni Firauni, inamtambua binadamu wa kweli, na kwa hiyo Mitume wa Mwenyezi Mungu wanapokuja kupambana na Firauni, jambo la kwanza wanalojaribu ni kuamsha ule ubinadamu wa ndani ulio ndani yake umpinge yeye mwenyewe. Ana fitra inayomfahamu Mwenyezi Mungu; ana ufahamu wa Mungu wake katika kina cha dhamiri yake. Ukanushaji na mashaka yote ni maradhi na upotovu kutoka kwenye asili halisi ya binadamu.