Picha zinazoonyesha viatu na koti la Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, huku zikitumiwa kuonyesha maisha yake ya unyenyekevu na kutopenda anasa licha ya kushika nafasi ya juu ya uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maelfu ya viatu vya watoto na picha za waandishi wa habari waliouawa Gaza zimeoneshwa katika uwanja wa Den Bosch nchini Uholanzi katika tukio la kumbukumbu lililolenga kuwakumbuka zaidi ya watoto 21,000 waliopoteza maisha na kulaani ukimya wa kimataifa kuhusu janga hilo.