Vikuu
-
Kivuli cha Nyaraka za Jeffrey Epstein juu ya Vyuo Vikuu vya Marekani
Nyaraka mpya kuhusu Jeffrey Epstein zimeibua athari kubwa katika vyuo vikuu vya United States, zikisababisha kusimamishwa kwa baadhi ya maprofesa, kufungwa kwa vituo vya utafiti, na kujiuzulu kwa viongozi, huku mjadala ukiibuka kuhusu uwazi wa ufadhili na uhusiano wa taasisi za elimu na wahisani wenye utata.
-
Maandamano Yatikisa Marekani, Minneapolis Kituo Kikuu cha Upinzani Dhidi ya ICE
Wimbi la maandamano linaendelea kuitikisa Marekani, huku jiji la Minneapolis likiwa miongoni mwa vituo vikuu vya upinzani dhidi ya operesheni za polisi wa uhamiaji (ICE). Maelfu ya raia wameingia mitaani wakipinga matumizi ya nguvu kupita kiasi, na maandamano yamesambaa hadi miji mingine kama Portland, Maine, San Francisco na Washington DC. Serikali iko chini ya shinikizo kubwa la ndani, huku wananchi wakidai haki, uwazi na kuheshimiwa kwa utu wa raia.
-
Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Asilimia 92 ya Watu wa Afghanistan Wanataka Elimu kwa Wasichana Kuendelezwa
Wakati Serikali ya Taliban inaendeleza sera za kuzuia elimu kwa wasichana, ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha wazi kuwa watu wa Afghanistan – wanawake kwa wanaume, wa mjini kwa vijijini – wanataka mabadiliko. Wanataka elimu kwa wasichana, fursa za kazi kwa wanawake, na mustakabali bora kwa jamii nzima.