Waandamanaji walibeba mabango na kuziba baadhi ya barabara wakitaka hatua za haraka za kimataifa kuchukuliwa. Baadaye maandamano hayo yalizingira mgahawa wa OWO, ambapo baadhi ya wabunge wa Uingereza waliripotiwa kuwa na kikao, kabla ya kumalizika kwa amani kufuatia kuwasili kwa Polisi.
Wakati mbio kubwa za baiskeli nchini Hispania zilikumbwa na vurugu za waandamanaji waliopinga ushiriki wa timu ya Israel, mataifa kadhaa ya Ulaya yametishia kususia tukio maarufu la burudani endapo Israel itaruhusiwa kushiriki.
Kufuatia maandamano ya Uturuki yaliyotokana na kukamatwa kwa Meya wa Istanbul, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametangaza kukamatwa kwa watu 343 katika majimbo 9 ya nchi hiyo.