Adui wetu wa wanadamu ni shetani; naye pia ana wafuasi wanaomsaidia. Wafuasi hao wana majina na majukumu mbalimbali, ambayo tutayataja katika makala hii.
Qur’ani katika asili ya kila binadamu, hata kama ni Firauni, inamtambua binadamu wa kweli, na kwa hiyo Mitume wa Mwenyezi Mungu wanapokuja kupambana na Firauni, jambo la kwanza wanalojaribu ni kuamsha ule ubinadamu wa ndani ulio ndani yake umpinge yeye mwenyewe. Ana fitra inayomfahamu Mwenyezi Mungu; ana ufahamu wa Mungu wake katika kina cha dhamiri yake. Ukanushaji na mashaka yote ni maradhi na upotovu kutoka kwenye asili halisi ya binadamu.