Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlulbayt (a.s) akizungumzia hali ya sasa ya dunia:
Ameyasema kwamba jamii ya binadamu leo inakabiliwa na umasikini, ubaguzi, ukosefu wa haki, ujinga, upuuzi na ukoloni wa kihisia. Masuala haya yamezua wasiwasi mkubwa.
Aidha, tabia ya ukatili imeibuka katika baadhi ya jamii, na matukio ya uvunjaji wa haki, mauaji na vurugu yameenea.
Msemo huu: "Elimika Usiwe Msomi" ni wito wa kuhusisha Elimu na Maadili. Elimu ya Kweli huonekana katika namna unavyowatendea wengine. Namna unavyofikiri kuhusu Haki na Uadilifu kwa kila Mwanadamu bila kujali Imani yake ya Kidini.