Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Sugiono, mjini Mashhad, wakati ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Indonesia ukiendelea na ziara ya kutoa rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Balozi wa Iran nchini Iraq, Mohammad Kazem Al-Sadeq, amekutana na Patriarki (Baba-Kiongozi) mpya wa Kanisa la Kaldania, Mar Paulus III Nona, jijini Baghdad ambapo pande hizo zimesisitiza umuhimu wa kuimarisha maelewano ya kijamii, kuishi kwa amani kati ya dini mbalimbali na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.
Ayatollah Abul-Qasim Alidoust, mmoja wa walimu wa masomo ya kiwango cha juu (Dars-e-Kharij) katika Hawza ya Kiislamu ya Qom, amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatollah al-Uzma Javadi Amoli