Iran yazindua miradi mitano ya kimkakati ya sekta ya mafuta na gesi yenye thamani ya dola milioni 350, inayolenga kuongeza uzalishaji wa gesi asilia hadi mita za ujazo milioni 32 kwa siku, kuimarisha miundombinu ya nishati na kupunguza gesi zinazopotea kutokana na uchomaji.
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, akihutubia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jukwaa la Nchi Zinazouza Gesi Asilia, uliofanyika jijini Moscow, alitoa heshima kwa kumbukumbu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Ali Khamenei (Marehemu), akisisitiza kuwa mipango na uungwaji mkono wake vilikuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha jukwaa hilo.
Aidha, akizungumzia matokeo ya mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, Pezeshkian alisema kuwa vikwazo vya upande mmoja pamoja na kuzingirwa kwa njia za baharini na angani kwa nchi hiyo ni tishio kwa uthabiti wa masoko ya nishati. Alitoa wito wa kulaani hatua hizo na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana nazo.