Abdulrahman Mohammed al-Sayed, mgombea wa Chama cha Democratic, ameshinda uchaguzi katika jimbo la Michigan dhidi ya Mike Rogers, mgombea wa Chama cha Republican, na hivyo kutambuliwa kuwa Mwislamu wa kwanza kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Seneti la Marekani.
Ushindi wake wa kihistoria umepatikana katika mazingira ambayo Donald Trump na baadhi ya viongozi wa Republican walikuwa wamemshambulia mara kadhaa wakati wa kampeni za uchaguzi kwa sababu ya imani yake ya kidini.