eid ghadir
-
Ayatullah Ramadhani: Bila ya Ghadir, Dini Ingepotoshwa Tangu Miaka ya Kwanza
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kusisitiza nafasi ya kimkakati ya tukio la Ghadir katika kulinda asili na usafi wa dini, alisema: "Kama lisingekuwepo tukio la Ghadir, basi dini ingeweza kupotoshwa tangu miaka ya mwanzo."
-
Wito wa Kwanza | Tamasha la Kitaifa la Ushairi wa Ghadir Kufanyika Katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa Foundation - Mbezi Beach - Dar-es- Salaam
Washairi wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali watahudhuria kwa ajili ya kusoma mashairi yanayogusa nyoyo kuhusu: Tukio la Ghadir, Mapenzi kwa Ahlul-Bayt(as), na mafundisho ya Kiislamu.
-
Maana ya Ghadir Khum na Umuhimu wa Siku ya Ghadir Khum katika Uislamu
Ghadir Khum ni tukio la kihistoria lenye uzito mkubwa kwa Waislamu, hasa kwa wale wanaotilia mkazo nafasi ya Ahlul Bayt (a.s) katika uongozi wa umma. Ni siku ya kutafakari juu ya uongozi wa haki, kutambua mafundisho ya Mtume (s.a.w.w), na kuhuisha uhusiano wa kidini kwa msingi wa upendo, uadilifu, na utiifu kwa uongozi wa kweli wa Kiislamu.
-
Kwa upendo wa Wilayat ya Amirul Muuminina (a.s); Sherehe za Umma za Ghadir zinafanyika katika zaidi ya miji 500 na nchi 20 duniani kote
Msemaji wa Kamati ya Sherehe za Umma za Ghadir Khumm alisema kuwa sherehe hii imeenea kwa zaidi ya miji 500 nchini Iran na katika nchi 20 duniani. Mwaka huu, tunatarajia kupika zaidi ya sufuria 30,000 za chakula cha moto, kushirikishwa kwa zaidi ya watumishi 100,000 mjini Tehran, kuwepo kwa mabaraza (Mawa'qib) ya umma 2,400 na kuanzishwa kwa mbuga za michezo kwa watoto milioni moja; yote haya kwa upendo wa Wilaya ya Amirul Momineen (a.s).
-
Tangazo la Sala ya Eid:
Eid Al_Fitri yatangazwa Tanzania kabla ya kuonekana kwa Mwezi
Mtume (s.a.w.w) ametuelekeza akisema: "Fungeni kwa kuonekana (kwa kuuona) Mwezi, na Fungueni kwa Kuonekana Mwezi". Hivyo tunatarajia kuonekana kwa Mwezi itakuwa ni tarehe 30 au 31".