Filamu ya Iran “Maula” iliyoongozwa na Abbas Lajvardi imetambulishwa kama kazi ya kipekee katika Tamasha la 44 la Filamu la Fajr, ikiwa ndiyo filamu pekee iliyozalishwa kwa kiwango kikubwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI), na kutajwa kuwa hatua ya kihistoria kwa Tasnia ya sinema ya Iran na dunia.
Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kupitia Tamko la Baku limesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha sekta za ubunifu na diplomasia ya kitamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu.