Miradi mikubwa yenye thamani ya mabilioni imetekelezwa katika mikoa mbalimbali, huku maboresho ya kiutawala na ya kimuundo yakifanikishwa, ikiwemo kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti, JUWAKITA na JUVIKIBA, pamoja na mabadiliko ya Katiba ya BAKWATA ili kuendana na mahitaji ya sasa.
Sambamba na kuwadia kwa siku ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), hafla ya kuadhimisha siku hii ilifanyika katika Kituo cha Fiqhi cha Maasemamu Watakatifu (a.s) upande wa magharibi mwa jiji la Kabul. Washiriki, sambamba na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imam Hussein (a.s), walitoa malalamiko makali dhidi ya ukosefu wa uratibu wa kisiasa na kisheria ambao mwaka huu uliwazuia waumini wengi wa Afghanistan kusafiri kwa wingi kwenda Karbala.