Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Majid Ibn al-Reza, amesema nguvu ya ulinzi ya Iran inalenga kuimarisha uwezo wa kuzuia vita na kuhakikisha nchi inalindwa, si kuanzisha vita au uchokozi dhidi ya mataifa mengine.
Shirika la Ujasusi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukulia hatua yoyote ya kuvuka mipaka myekundu nchini Lebanon na Gaza kuwa sawa na kutangaza vita vya moja kwa moja dhidi yake, huku likisisitiza utayari wake wa kuchukua hatua za kujihami na kufungua nyanja mpya za mapambano ikiwa hali hiyo itatokea.