Baadhi ya waliokuwa huru wamesema kuwa walikutana na Walebanon waliokuwa wameorodheshwa awali kama waliopotea katika magereza ya Ofer, Nafha, Ramla, na Ashkelon.
Mazungumzo kati ya Hamas na Mamlaka ya Misri Mjini Cairo yanaendelea kufanikisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza. Makubaliano hayo yanajumuisha kuachiliwa kwa idadi kadhaa ya wafungwa wa Israel na Palestina na iwapo yatakubaliwa, yanaweza kusaidia kuboresha hali ya kibinadamu katika eneo hilo. Walakini, Tel Aviv bado haijajibu vyema kwa makubaliano ya mwisho.