Shirika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa hadi sasa hakuna majeruhi walioripotiwa katika hafla ya kuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, licha ya mamilioni ya waombolezaji kushiriki. Shirika hilo limeeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi mzuri wa tukio hilo pamoja na ushirikiano wa wananchi.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amejibu ukosoaji wa kimataifa kuhusu nafasi ya nchi yake katika mgogoro unaoendelea wa Gaza, akisisitiza kuwa jukumu lake kuu ni kulinda usalama na afya ya watu wa Misri, na kwamba nchi yake “inajilinda tu.”