Profesa mashuhuri wa vyuo vya kidini vya wanawake, katika hafla ya uzinduzi wa mwaka mpya wa masomo, alivitaja “ikhlasi na uchamungu (taqwa)”, “kuungana na uongozi wa Kiislamu (wilaya)”, na “kuzingatia haki za wengine” kuwa ni nguzo tatu muhimu za mafanikio kwa wanafunzi wa fani za dini.
Akaeleza kwa msisitizo kuwa: Taasisi za kielimu za wanawake zinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu kwa wanawake wa ulimwengu wa Kiislamu, na kutumia uwezo huo kwa ajili ya kusambaza maarifa ya Kiislamu katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.