Hussein Jaberi Ansari amesema suala la Iran sasa linaangaliwa kwa mtazamo wa maslahi ya juu ya taifa, huku akisisitiza kuwa uwezo wa kujihami wa nchi hiyo unajumuisha nyanja za kijeshi, kitamaduni, kijamii na kimedia.
Imam Khamenei amesema Iran inalengwa na Marekani kutokana na utajiri wake wa asili na nafasi yake ya kijiografia, akibainisha kuwa mafuta, gesi na madini ya thamani ni miongoni mwa vivutio vinavyoifanya Iran kuwa shabaha ya tamaa ya kibeberu. Kauli hiyo aliitoa wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.