Kulinda umoja wa ardhi na kuzingatia utambulisho wa kidini ni miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakipewa umuhimu mkubwa na viongozi wa kidini katika ardhi za Kiislamu. Kiasi kwamba kila aina ya uvamizi au shambulio dhidi ya ardhi za Kiislamu ilikabiliwa na mwitikio mkali kutoka kwao. Uvamiuzi wa Azarbaijan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na juhudi za kuutenga mkoa huo kutoka Iran ni miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha tena ushawishi wa uongozi wa kidini katika kulinda umoja wa ardhi ya nchi. Aidha, kulinda utambulisho wa kitaifa wa Kiairani pia lilikuwa ni mojawapo ya masuala yaliyopatiwa umuhimu maalum na viongozi (Marajii) wa kidini katika kipindi cha utawala wa Pahlavi.