Mamlaka ya DCEA imekamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilo 20.03 zilizofichwa kwenye balo la mitumba ndani ya bus la Scania la King Masai Tours, lenye namba za usajili AAM 297 CA, likisafiri kati ya Nampula, Msumbiji na Dar es Salaam. Watuhumiwa waliokamatwa ni Amasha Iddi Mrisho (40) kutoka Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32) raia wa Msumbiji. Uchunguzi na kesi za kiutumishi zinaendelea.