ukiukaji
-
Serikali ya Iran Yalaani Mashambulizi dhidi ya Raia Sereki na Kuyataja kuwa Ukiukaji Mkubwa wa Sheria za Kimataifa
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mashambulizi yaliyowalenga raia katika eneo la Sereki, kusini mwa Iran, ikisema kuwa mashambulizi hayo pamoja na shambulio la awali dhidi ya shule ya Minab, lililosababisha vifo vya wanafunzi, ni ukiukaji mkubwa wa misingi ya kibinadamu na sheria za kimataifa.
-
Chanzo cha Kijeshi Yemen: Aramco Najran Yalengwa kwa Ndege Isiyo na Rubani
Chanzo cha kijeshi Yemen kimesema shambulio dhidi ya Aramco Najran lilikuwa ni jibu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uvamizi wa anga la Yemen na ndege za kijeshi za Saudi Arabia.
-
Jeshi la Yemen Latangaza Kushambulia Lengo la Kijeshi katika Uwanja wa Ndege wa Najran
Jeshi la Yemen limesema limelenga shabaha nyeti katika Uwanja wa Ndege wa Najran kwa kutumia ndege isiyo na rubani, likieleza kuwa operesheni hiyo ilikuwa jibu kwa kile lilichodai kuwa ni ukiukaji wa anga la Yemen na ndege zisizo na rubani za Saudi Arabia.
-
Iran Yalaani Mashambulizi Yanayodaiwa Kufanywa na Marekani na Saudi Arabia dhidi ya Iraq na Misafara ya Mazuwwari wa Arbaeen
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Marekani na Saudi Arabia dhidi ya maeneo rasmi nchini Iraq na misafara ya kuhudumia mazuwwari wa Arbaeen ya Imam Hussein (as), ikiyataja kuwa ni ukiukaji wa mamlaka ya Iraq na sheria za kimataifa.
-
Walinzi wa Mapinduzi wa Iran: Kumetokea Mlipuko Katika Meli Mbili za Mafuta Katika Mlango Bahari wa Hormuz
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran wamesema meli mbili za mafuta zililipuka na kusimama baada ya kujaribu kutumia njia iliyotajwa kuwa si salama na yenye hatari katika Mlango Bahari wa Hormuz.
-
Rais Pezeshkian: Marekani Inakiuka Sheria katika Siasa na Michezo, Iran Itatetea Haki Zake
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema ukiukaji wa sheria na udanganyifu ni sifa zinazotawala mwenendo wa Marekani katika siasa na michezo, akisisitiza kuwa Iran haitakubali vitendo hivyo na itaendelea kutetea haki zake kwa uthabiti.
-
Iran: Mashambulizi ya Marekani Kusini mwa Nchi Yathibitisha Kutoheshimu Ahadi za Kimataifa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya vituo vya ufuatiliaji kusini mwa Iran, ikisema kuwa hatua hiyo inaonesha wazi kwamba Washington haithamini wala kuheshimu ahadi na wajibu wake wa kimataifa.
-
Iran Yafunga Mlango wa Bahari wa Hormuz; Yaanza Hatua za Kujibu Ukiukaji wa Makubaliano na Marekani na Israel
Khalil Nasrallah: Iran yafunga Mlango wa Bahari wa Hormuz kama hatua ya kwanza ya kujibu ukiukaji wa makubaliano unaodaiwa kufanywa na Marekani na Israel; sasa mpira uko kwa Donald Trump.
-
Madaktari Wasio na Mipaka: Takriban watu 82,000 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Lebanon
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limetangaza kuwa mgogoro wa kibinadamu nchini Lebanon haujaisha hata baada ya mwaka mmoja tangu vita, na zaidi ya watu 82,000 bado ni wakimbizi wa ndani. Ukiukaji unaoendelea wa Israel unazuia watu hawa kurejea makwao.