23 Septemba 2025 - 12:45
Madaktari Wasio na Mipaka: Takriban watu 82,000 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Lebanon

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limetangaza kuwa mgogoro wa kibinadamu nchini Lebanon haujaisha hata baada ya mwaka mmoja tangu vita, na zaidi ya watu 82,000 bado ni wakimbizi wa ndani. Ukiukaji unaoendelea wa Israel unazuia watu hawa kurejea makwao.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Darwin Diaz, mratibu wa kitiba wa Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini Lebanon, leo katika taarifa kwa vyombo vya habari alisema:

"Mwaka mmoja umepita tangu kuongezeka kwa vita vya Israel dhidi ya Lebanon, na licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Novemba uliopita, vita bado havijaisha na mgogoro wa kibinadamu haujamalizika.
Zaidi ya watu 82,000 bado ni wakimbizi wa ndani, na maelfu ya familia zinahangaika kupata huduma za afya, huku zikijaribu kujenga maisha yao upya katika hali ya sintofahamu."

Kwa mujibu wa Russia Al-Youm, taarifa hiyo imeeleza kwamba:

Mashambulizi ya karibu kila siku ya Israel dhidi ya Lebanon, pamoja na uvamizi wa maeneo ya mpaka wa kusini, yamekuwa kizuizi kikubwa kwa wakimbizi kurejea nyumbani.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa:

"Katika kusini mwa Lebanon, vita vimeharibu miundombinu, ikiwemo huduma za afya.
Katika kipindi cha kilele cha mapigano, hospitali 8 – nyingi zikiwa katika maeneo ya kusini – zililazimika kufungwa au kuhamishwa.
Hospitali 21, takriban asilimia 13 ya hospitali zote nchini, ziliharibiwa, zikafungwa au zikapunguza huduma kwa kiwango kikubwa."

Imeongezwa pia kuwa:

"Vituo 133 vya huduma za afya ya msingi vimefungwa, na mkoa wa Nabatieh umepoteza asilimia 40 ya uwezo wake wa hospitali.
Kwa sasa, vituo vingi vilivyoathirika bado havijafunguliwa, na vingine vinahitaji ukarabati mkubwa."

Madaktari Wasio na Mipaka wametilia mkazo kuwa:

"Kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za afya ya mwili, akili na misaada ya kibinadamu nchini Lebanon, timu zetu zitaendelea kutoa huduma popote inapohitajika, na kuhakikisha kuwa watu wote – Walebanon, wakimbizi na wahamiaji – wanapata huduma muhimu za afya."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha