Mwenyezi Mungu ametajwa katika Qur’ani Tukufu kuwa ni “Mbora wa Watoaji wa Riziki.”
Riziki ambazo watu huwapa wengine zimechanganyika na mapungufu mengi; ni zenye mipaka na za muda mfupi, na hakuna uhakika wa kuendelea kwake katika siku zijazo. Wakati mwingine huambatana na kudai fadhila, na wakati mwingine huambatana na kumdhalilisha anayepokea au kutarajia malipo ya aina fulani kwa kile alichotoa.
Hali ni tofauti na riziki ya Mwenyezi Mungu; haina mipaka wala ukomo, hakuna hofu kuhusu mustakabali wake, wala haina kudai fadhila au matarajio ya malipo. Bali, mwanadamu hupewa riziki tangu anapowekwa tumboni mwa mama yake hadi katika dakika ya mwisho ya maisha yake. Na hata Siku ya Kiyama, riziki hiyo itaendelea kuwepo kwa watu wanaostahiki, katika kiwango cha juu na kilicho bora zaidi.