Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamehoji taarifa zinazokinzana kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran, baada ya baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa umedhoofika pakubwa huku matukio ya baadaye yakionyesha Iran ikiendelea na operesheni za kijeshi, hali iliyozua mjadala kuhusu ukweli wa taarifa hizo.
Video ya hotuba ya Rais wa Marekani katika kikao kilichofanyika Miami, ambapo alitumia mtindo wa utani akimtaja Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, imesambaa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua maoni na mjadala mkali miongoni mwa watumiaji.