31 Desemba 2024 - 04:05
Muhammad; Jina maarufu na linalopendwa zaidi kwa Watoto wa kiume wachanga (wanapozaliwa) katika Mji Mkuu wa Ujerumani

Kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Jina la Kiislamu "Muhammad" lilikuwa Jina maarufu na lenye kupendwa zaidi kwa watoto wa kiume (wachanga) pindi wanapozaliwa katika Jiji la Berlin, Mji Mkuu wa Ujerumani, katika mwaka wa 2024.

Mnamo mwaka 2023, Jina Muhammad lilitambuliwa pia kama Jina maarufu na lenye kupendwa zaidi kwa watoto wa kiume katika Jiji la Berlin. Majina "Mateo na Elias" katika mwaka wa 2023 na 2024 yalikuwa majina ya pili na ya tatu kuwa maarufu na kupendwa katika Jiji hili.

Zaidi ya wahamiaji Waislamu milioni 5.5 wanaishi Ujerumani, Uislamu ni Dini ya Pili kwa ukubwa nchini humo, na Waislamu ni takriban 5% ya wakazi wa Ujerumani.