Ali Baraka Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Kitaifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nje ya Palestina amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) na kamandi kuu ya PFLP chini ya uongozi wa Abu Imad Ramez Naibu Katibu Mkuu wa harakati hiyo.
Katika mazungumzo hayo, ambayo yalihudhuria pia na Abu Kifah Ghazi mwakilishi wa ofisi ya kisiasa na afisa wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) huko Lebanon; pande mbili zimeitaka jamii ya kimataifa kulaani mashambulizi ya utawala wa kizayuni na kuchukua hatua ili kusitishwa vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Palestina.
Harakati ya Hamas imesisitiza katika taarifa yake kuwa pande mbili zimechunguza matukio ya karibumi kuhusu kadhia ya Palestina hasa mashambulizi mapya ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Hamas na harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina zimesisitiza kuwa adui Mzayuni ametenda jinai ya mauaji ya kinyama dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Palestina na kuua shahidi Wapalestina zaidi ya 450.
Harakati mbili hizi za Palestina zimewataka wasuluhishi kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuushinikiza utawala ghasibu wa Israel ambao ndio uliokiuka makubaliano ya kusimamisha mapigano uliyoyasiani wenyewe Januari 17 mwaka huu.
342/
Your Comment