Avigdor Lieberman amekiri katika mahojiano na gazeti la Ma'ariv kwamba Israel imepoteza kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya makadirio yake ya kifedha wakati wa vita vya hivi majuzi.
Ameongeza kuwa kusitishwa kwa uchumi wa Israel kumeugharimu utawala huo shekeli bilioni 1.5 (dola milioni 403) katika Pato la Taifa kwa kila siku ya vita.
Wakati huo huo, makadirio ya awali ya uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran kwa muda wa siku 12 tu yanaonyesha kuwa Tel Aviv imepata hasara ya moja kwa moja ya zaidi ya dola bilioni 5. Takwimu hii inajumuisha uharibifu wa miundombinu, majengo, pamoja na misaada ya kifedha kwa makampuni yaliyoathirika.
Kwa upande mwingine, Wizara ya Fedha ya Israel imekadiria katika ripoti ya ndani kwamba jumla ya gharama za vita, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mifumo ya ulinzi na silaha, kujaza risasi, na shughuli za msaada, zitafikia dola bilioni 12.
342/
Your Comment