Wiki iliyopita, magaidi waliopata himaya ya Israel na Marekani, walijipenyeza katika maandamanao ya amani ya wananchi na kuiharibu mali za umma na binafsi katika miji kadhaa nchini Iran, na kusababisha vifo vya raia na maafisa wa usalama pamoja na kuwajeruhi wengine.
Mnamo Januari 12, wananchi katika maeneo mbalimbali ya Iran walijitokeza kwa wingi kulaani machafuko hayo na vitendo vya kigaidi, wakirejea upya utiifu wao kwa Mapinduzi ya Kiislamu na kukemea wale wanaotuhumiwa kuvuruga utulivu wa taifa.
Katika taarifa yake, Jukwaa la Umoja na Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Duniani limesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ni wahusika wakuu katika kuchochea machafuko hayo.
Habari inayohusiana:
Wanazuoni wa ulimwengu wa Kiislamu watoa tamko dhidi ya Trump huku wakimuunga mkono Imam Khamenei
Taarifa hiyo pia iligusia matukio ya kudhalilishwa kwa Qur’ani Tukufu na kuvunjwa kwa misikiti wakati wa machafuko, ikisema kuwa maadui ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakisukuma ajenda ya chuki dhidi ya Uislamu sasa wamevua barakoa na kutukana waziwazi matukufu ya dini kupitia vibaraka wao.
WFPIST ilisema kuwa uungaji mkono uliotolewa na wanazuoni na wasomi wa Kishia na Kisunni kwa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa machafuko ya hivi karibuni ni jambo la kuthaminiwa na kupongezwa.
Pia ililisifu taifa la Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano makubwa ya kulaani machafuko hayo.
Your Comment