24 Desemba 2014 - 19:25
Israel na Hamas wapambana vikali

Jeshi la Isreal limesema limetumia vifaru na ndege kufanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza, baada ya wanajeshi wake waliokuwa wakifanya doria kwenye kuvuka mpaka na kushambuliwa na watunguaji wa kipalestina.

Jeshi hilo limesema askari wake mmoja kutoka kikosi cha Bedouin amejeruhiwa vibaya na watunguaji hao. Msemaji wa jeshi la Israel Luteni Kanali Peter Lerner amesema mashambulizi hayo ambayo amesema ni ya pili wiki hii, ni ukiukaji mkubwa wa mipaka ya taifa la Israel, na kuongeza kuwa hawatasita hata kidogo kujibu mashambulizi yanayohatarisha maisha ya wanajeshi wa Israel.

Kundi la Hamas ambalo linautawala Ukanda wa Gaza limesema mwanamgambo wake mmoja ameuawa, kamiloi halikutoa maelezo zaidi.

Jeshi la Israel limekuwa likikiuka kanuni za kimatafa nakuingia kwenye mipaka ya Palestina bila ya idhini, wanamgambo wa Hamas kwasasa wanakadiriwa kuwa na nguvu na maandalizi ya hali ya juu ya kukabiliana na jeshi la Israel, hii inatokana na mafunzo na msaada wa silaha ulizopata kutoka kwaJamhuri ya kiislamu ya Iran.

Tags