Msemaji wa Umoja wa Ulaya Susanne Kiefer amesema umoja huo utakata rufaa kuhusiana na uamuzi uliotolewa na mahakama ya umoja wa Ulaya mwezi Desemba mwaka jana wa kuagiza kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas kuondolewa kutoka orodha ya makundi ya kigaidi. Kiefer amesema mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana leo mjini Brussels, Ubelgiji wamekubaliana katika mkutano huo kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Katika uamuzi wake mahakama hiyo ilisema kuorodheshwa kwa Hamas kama kundi la kigaidi kulitegemea ripoti za vyombo vya habari na sio uchunguzi wa kina.
Hatua ya Hamas kutolewa kwenye orodha ya magaidi iliichukiza sana serikali ya Israel, ambayo ni hasimu mkuu wa kundi hilo la wapigania haki za wapalesatina.