-
Utafiti mpya wa kila mwaka, uliochapishwa jana Jumatatu, unaonyesha kuwa mtazamo wa kimataifa kuhusu Marekani umerudi nyuma kwa kiasi kikubwa katika m
Maelfu ya watu waliandamana katika mitaa ya Paris na miji mingine ya Ufaransa siku ya Jumapili kulaani ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na kumuenzi Aboubakar Cissé, kijana kutoka Mali aliyeuawa akiswali ndani ya msikiti.
-
Uchunguzi wa maoni: Sura ya Marekani imeporomoka duniani kote
Utafiti mpya wa kila mwaka, uliochapishwa jana Jumatatu, unaonyesha kuwa mtazamo wa kimataifa kuhusu Marekani umerudi nyuma kwa kiasi kikubwa katika mwaka uliopita, na kwamba mtazamo wa watu kuhusu nchi hiyo sasa ni mbaya zaidi ikilinganishwa na Uchina.
-
FAO yabainisha hofu kuhusu kukaribia baa la njaa Gaza huku Israel ikiendeleza jinai
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) lilionya Jumatatu kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuongezeka katika Ukanda wa Gaza, likieleza hatari ya njaa inayokaribia, kuporomoka kwa sekta ya kilimo, na kuzuka kwa magonjwa hatari huku utawala dhalimu wa Israel ukiendeleza mzingiro na jinai katika eneo hilo la Wapalestina.
-
Jenerali wa zamani aonya: Israel imegeuka kutoka kuwa mali na kuwa mzigo kwa Marekani
Kamanda wa zamani wa jeshi la Israel huko Gaza amesema Israel sasa imegeuza kutoka kuwa mali na kuwa mzigo mzito kwa Marekani.
-
Kukandamizwa watetezi wa Palestina na kuporomoka maadili ya kibinadamu barani Ulaya
Uwanja wa Stalingrad wa Paris hivi karibuni ulishuhudia maandamano makubwa ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Rais Trump wa Marekani awasili Saudia, alenga kutoka na kitita cha dola trilioni 1
Rais wa Marekani, Donald Trump, amewasili mjini Riyadh katika awamu ya kwanza ya ziara yake ya siku nne katika eneo la Asia Magharibi, ambapo analenga kupata hadi dola trilioni moja za uwekezaji kutoka Saudi Arabia.
-
Hamas yailaani Israel kwa kumuua mwandishi mashuhuri wa habari Gaza
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imelaani vikali kitendo cha utawala haramu wa Israel cha kumuua mwandishi habari maarufu na mwenye ushawishi mkubwa wa Kipalestina na kuyataka mauaji hayo kuwa ya kinyama. Hamas imesema mauaji hayo ni sehemu ya kampeni ya Israel kunyamazisha vyanzo vya ukweli.
-
Mauzo ya tende za Iran nje ya nchi yapindukia dola milioni 205 kwa mwaka
Iran iliuza tende zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 205 katika mwaka wa kalenda wa Kiirani wa 1403 (uliomalizika Machi 20, 2025), kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka Mamlaka ya Forodha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRICA), ikionyesha nafasi imara ya nchi hii katika soko la kimataifa la tende.
-
Iran kujiunga na safu ya watengenezaji wa ndege za kibiashara duniani
Sambamba na maendeleo ya mradi wa uundaji wa ndege ya kwanza ya jet ya Iran ya kubeba abiria 8, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni itajiunga na kundi dogo la watengenezaji wa ndege za kibiashara duniani.
-
Mkutano wa 31 wa Nyuklia wa Iran wafunguliwa mjini Mashhad
Mkutano wa 31 wa Nyuklia wa Iran, ulioandaliwa na Jumuiya ya Nyuklia ya Iran na kuungwa mkono na Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI), umefunguliwa katika mji wa Mashhad, uliopo kaskazini-mashariki mwa Iran.
-
Katika Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu Tehran, tafsiri ya wasifu wa Shahidi Jenerali Qasem Soleimani itazinduliwa rasmi
Katika Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran, vitabu vitatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kazakhi vitazinduliwa rasmi, na miongoni mwao ni kitabu kiitwacho "Rafiki Yetu Mwenye Bahati", ambacho ni wasifu wa Shahidi Jenerali Qasem Soleimani.
-
Ijue Siri ya Majina ya Heshima (Lakabu) ya Imamu Ridha (a.s) _ (1)
Majina haya ya heshima (Lakabu) hayakuwa tu kwa lengo la kuitana (ili mradi kuitana, pasina kuwepo kigezo chochote cha msingi), bali yalibeba taarifa za kiroho, madhumuni ya uongozi wa ki_Mungu, na mafunzo kwa Waislamu wote. Kujifunza kuhusu laqabu za Imamu Ridha (a.s) ni kujifunza kuhusu maisha na tabia bora za Kiislamu.
-
Dola bilioni 8: Gharama ya kashfa (fedheha) na mashambulizi yaliyoshindwa ya Marekani nchini Yemen
Vyombo vya habari vya Marekani vimekadiria gharama ya mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Yemen, katika muktadha wa kuunga mkono Israel, kufikia dola bilioni 8. Vimeripoti kuwa Trump alikuwa akimkejeli Biden kwa sababu ya gharama za vita dhidi ya Yemen, lakini yeye mwenyewe alisababisha hasara kubwa zaidi, huku Serikali ikificha takwimu halisi za vifo.
-
Donald Trump awasili katika Mji Mkuu wa Saudi Arabia / Kuanza kwa ziara ya kikanda ya Rais wa Marekani
Rais wa Marekani, katika mwanzo wa ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi, amewasili katika jiji la Riyadh.
-
Kufanyika kwa Tamasha la Ushairi wa Amani katika mji wa Parachinar, Pakistan / Mkutano wa washairi wa Kishia na Kisunni wenye ujumbe wa umoja
Washairi Mashuhuri wa Kishia na Kisunni kutoka maeneo yote ya Kurram wamekusanyika katika tamasha lenye mada ya amani lililofanyika katika mji wa Parachinar, Pakistan.
-
Mkutano wa kihistoria wa Marjaa wa Kidini:
Najaf Ashraf: Ayatollah Jawadi Amuli akutana na Ayatollah Sistani / Zawadi ya Qur'an yatolewa katika Mkutano wa Viongozi hawa wawili wa juu wa Kidini
"Ayatollah al-Udhma Jawadi Amuli — ambaye yuko ziarani nchini Iraq kwa ajili ya kutembelea maeneo matakatifu — amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatollah al-Udhma Sistani huko Najaf Al-Ashraf."