Onyo hili linakuja baada ya ripoti ya hivi karibuni inayoonyesha kwamba idadi yote ya watu wa Gaza – takriban watu milioni 2.1 – wako katika "hatari kubwa ya njaa," baada ya miezi 19 ya vita, uhamishaji, na vikwazo vya misaada.
Kutoka Aprili 1 hadi Mei 10, asilimia 93 ya watu, watu 1.95 milioni wa Gaza, walikadiriwa kuwa katika hali mbaya zaidi ya ukosefu wa chakula.
Kwa kipindi cha Mei hadi Septemba, ripoti inatarajia kwamba Wagaza wote watakuwa wanahitajia misaada ambapo watakuwa wanakaribia mauti iwapo hawatapa misaada.
Mkuu wa FAO, Qu Dongyu amesema katika taarifa kwamba: "Jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua sasa. Kurudisha mara moja ufikaji wa misaada ya kibinadamu wa kiwango kikubwa ni muhimu." Aidha ameonya kwamba "kila ucheleweshaji unaongeza njaa na kutufanya tuwe karibu na janga la njaa."
FAO, katika taarifa hiyo, pia imeonyesha wasiwasi kuhusu kuporomoka kwa sekta ya kilimo Gaza.
Kabla ya vita, asilimia 42 ya ardhi ya Gaza ilikuwa inalimwa. Lakini uchambuzi wa pamoja wa FAO-UNOSAT (Kituo cha Satelaiti cha Umoja wa Mataifa) unaonyesha kwamba asilimia 75 ya mashamba na mabustani ya matunda yameharibiwa au kuangamizwa, huku zaidi ya theluthi mbili ya visima 1,531 vya kilimo vikiwa havifanyi kazi tena.
Uzalishaji wa mifugo umekoma kabisa na huduma za mifugo zimesimamishwa. FAO imeongeza kuwa: "Bila chakula na vifaa vya mifugo, si tu kwamba wachungaji watapoteza vyanzo hivi muhimu vya chakula, bali pia wanyama wasio na matibabu wanatishia pakubwa afya ya umma."
Tangu Machi 2, Israel imefunga mipaka ya Gaza na kuzuia kuingia humo chakula, dawa na misaada ya kibinadamu. Hatua hiyo ya utawala katili wa Isarel imezidisha janga la kibinadamu lililokuwepo tayari katika eneo hilo.
Zaidi ya Wapalestina 52,800 wameuawa Gaza katika vita vya mauaji ya kimbari ambavyo utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha Oktoba 2023, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
342/
Your Comment