Mkusanyiko huo ulifanyika kufuatia uamuzi wa serikali ya Ufaransa kuvunja jumuiya ya "Palestina katika hali ya dharura", asasi kubwa zaidi ya kiraia inayounga mkono Palestina nchini humo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bruno Riteau ameamuru kuvunjwa kwa asasi hiyo, akidai kuwa "huchochea vurugu" na "kutishia usalama wa umma."
Lakini kiuhalisia, kinacholengwa si kueneza chuki, bali ni harakati za kiraia na kuongeza ufahamu wa umma kuhusu jinai za utawala wa Israel huko Gaza. Wakati gazeti la Guardian linaripoti, likinukuu vyombo vya kimataifa, kuhusu "njaa ya kuratibiwa," "milipuko ya mabomu ya kiholela," na "ushahidi wa wazi wa mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza, uamuzi wa serikali ya Ufaransa wa kunyamazisha sauti za watetezi wa Palestina sio tu kwamba ni ishara ya upendeleo wa kisiasa, bali pia ni kujiondoa wazi kutoka kwa madai ya kanuni za demokrasia na haki za binadamu. Kwa maneno ya Raphael Arnault mbunge wa mrengo wa kushoto wa bunge ni kuwa, "Ufaransa sio tu imejitenga na kanuni za jamhuri, lakini pia inaelekea kwenye dhulma ya kibaguzi na kushirikiana na ufashisti mamboleo."
Ukandamizaji dhidi ya watetezi wa Palestina barani Ulaya hauko Ufaransa pekee. Wauangaji mkono wa wananchi madhlumu wa Palestina nchini Ujerumani, Uingereza na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na Marekani wako katika hatari ya kufukuzwa katika vyuo vikuu, sehemu za kazi na iwapo ni wahajiri au wahamiaji pia wako katika hatari ya kufukuzwa nchini humo.
Nchini Ujerumani, zaidi ya wanaharakati 200 wa haki za binadamu na watetezi wa Palestina wamekamatwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hii ni pamoja na kwamba nchi hii inajulikana kuwa muuzaji mkubwa wa silaha kwa Israel katika Umoja wa Ulaya. Ripoti mpya ya siri ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm SIPRI inaonyesha kuwa asilimia 43 ya sehemu za ndege za kivita za F-35 zilizotumika katika milipuko ya Gaza zilitengenezwa katika viwanda vya Ujerumani.
Operesheni kubwa ya kukamatwa wafuasi wa Palestina nchini Ujerumani, kufutwa kwa vibali vya mikusanyiko, na hata kupigwa marufuku alama kama bendera ya Palestina katika baadhi ya majimbo, kunaonyesha kukita mizizi na kuongezeka himaya na uungaji mkono kwa wananchi wa Palestina jambo ambalo halijawafurahisha viongozi wa mataifa ya Ulaya.
Nchini Uingereza, huku mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Gaza yakiongezeka, vyuo vikuu vimetakiwa kufuatilia na kuzuia shughuli za makundi yanayoiunga mkono Palestina chini ya mashinikizo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya "kukabiliana na misimamo mikali." Huko Oxford na UCL, mikusanyiko ya wanafunzi imekabiliwa na vitisho vya kusimamishwa kazi, na baadhi ya maprofesa wanaoiunga mkono Palestina wamelengwa na kampeni za hujuma na za kuwachafua.
Ukandamizaji wa watetezi wa Palestina sio tu ni radiamali ya hapa na pale; bali zinaonyesha aina ya uanzishwaji wa kiitikadi katika ngazi ya utawala wa Ulaya ambayo inafafanua upya msaada kwa Palestina ndani ya mfumo wa usalama, vitisho na hata ugaidi. Kama Raphael Arnault, mbunge wa mrengo wa kushoto wa bunge la Ufaransa, alivyoonya katika mkutano wa hivi majuzi huko Paris, ambapo alisema: "Serikali ya Ufaransa inateleza aina ya udhalimu wa kibaguzi"; Udikteta ambao unachinja uhuru wa raia kwa jina la usalama, na dhamiri ya umma kwa jina la masilahi ya kijiografia.
Ukweli wa mambo ni kuwa, Ulaya haiwezi kwa wakati mmoja kudai kuilinda Ukraine dhidi ya "uchokozi wa Russia" na kuwa msaidizi wa wavamizi dhidi ya mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza. Undumakuwili huu hubeba ujumbe hatari, sio tu kwa watu wa eneo hilo, bali pia kwa vizazi vijavyo vya Wazungu ambao ni: Maadili hayafafanuliwa kwa mujibu wa kanuni, bali kwa mujibu wa washirika wa kimkakati.
Katika ngazi ya vyombo vya habari, tunashuhudia pia mipango maalumu iliyoenea ya udiriki wa umma. Uchambuzi wa maudhui uliofanywa na Taasisi ya Oxford ya Mafunzo ya Vyombo vya Habari unaonyesha kuwa, kanali kuu za habari za Ufaransa na Ujerumani zinaelezea upinzani wa Wapalestina kwa neno "ugaidi" katika asilimia 90 ya matukio.
Hii ni katika hali ambayo, ripoti huru, ikiwa ni pamoja na ripoti ya hivi karibuni ya Guardian, zinaonyesha matokeo ya timu za matibabu huko Gaza ambayo yanaonyesha matumizi ya silaha za kemikali za majaribio na majeshi ya Israel na mauaji ya halaiki ya Wapalestina. Undumakuwili na unafiki kama huo katika utangazaji wa vyombo vya habari unaonyesha jaribio la wazi la kupotosha ukweli wa hali halisi na kuhalalisha uhalifu wa kivita.
Ikiwa katika miongo iliyopita, harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ziliweza kuamsha dhamiri ya kimataifa, leo hii, harakati za kuunga mkono Palestina zinabeba ujumbe huo wa kihistoria. Lakini tofauti ni kwamba serikali zinazodai uhuru sasa ziko mstari wa mbele wa udhibiti, ukandamizaji, na kususia.
Bila shaka umefika wakati kwa wasomi, wanafikra na nguvu ya kiraia ya Magharibi kubainisha makosa ya kimaadili ya tawala za Ulaya na kuzingatia suala la kutetea Palestina sio tu kama jukumu la kibinadamu, lakini pia kipimo cha kubakia kwa dhamiri ya kisiasa ya Magharibi.
342/
Your Comment