-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Awasalimia Wakristo wa Jamii ya Armenia Katika Mkoa wa Isfahan +Picha
Ziara hii inadhihirisha jitihada za serikali za kuimarisha uhusiano na jamii za kidini zinazopungukiwa, na kusherehekea mila na desturi zao za kidini na kitamaduni.
-
Shughuli za Uenezi wa Elimu na Maarifa ya Dini Zinazofanywa na Mabanati Wanaosoma Madrasat Hazrat Zainab (SA) Wakati wa Likizo
Picha hizi ni kielelezo cha wazi na dhahiri cha matunda ya juhudi zinazofanywa katika kueneza elimu na maarifa kupitia Madrasat Zainab (SA), inayosimamiwa na Rais wake, Dkt. Ali Taqavi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amlinde, ampe nguvu, afya njema na tawfiq ya kudumu katika kuitumikia Uislamu na Waislamu.
-
Heshima na Unyenyekevu wa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa Wazee | Sala ya Ijumaa - Masjid Abdallah Rashid - Zanzibar
Rais Dkt. Mwinyi pia ameswali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa 'Abdallah Rashid', ikiwa ni hatua inayotekeleza utaratibu wake wa kawaida wa kusali katika Misikiti mbalimbali nchini, kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kudumisha mahusiano ya karibu kati ya Viongozi na Waumini.
-
Mufti Mkuu wa Tanzania:
"Qur’an Tukufu Inahimiza Amani Kama Msingi wa Maisha ya Mwanadamu | Tunajifunza Amani Kutoka Katika Kisa cha Nabii Ibrahim (as)
Katika kufafanua hoja yake, Mufti Mkuu wa Tanzania ametaja kisa cha wageni wa Nabii Ibrahim (as) kama kinavyosimuliwa ndani ya Qur’an Tukufu. Amesema kuwa wageni hao walipoingia nyumbani kwa Nabii Ibrahim (as), walimpa maamkizi ya amani, naye akajibu kwa maamkizi yale yale ya amani.