Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:25:29
1323749

Uhuru Kenyatta ziarani Goma huku waasi wa M23 wakijaribu kuuteka mji wa Kibamba

Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameutembelea mji wa Goma ambao ni makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wapiganaji wa kundi la M23 walikuwa wakipigana NA jeshi la taifa FARDC, kaskazini mwa mji huo.

Maafisa wa usalama na wakazi wa mji wa KibAmba wanasema wapiganaji wa M23 wameuzunguka mji huo uliopo kilomita 20 kaskazini mwa Goma wakipambana vikali na wanajeshi wa FARDC.

Mpatanishi wa JumuiYAa ya Afrika Mashariki EAC, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, alikuwa katika kambi ya Kanyaruchinya, wakati uvumi wa wapiganaji kusonga mbele ulikuwa unaenea.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Goma, Uhuru Kenyatta alisema: Nimesikia hadithi za kuvunja moyo, siwezi kupuuza kile nilichokishuhudia. "Ni lazima niwaambie wote wanaohusika kwamba hamuwezi kujadiliana mnapokabiliwa na janga la kibinadamu." 

Kabla ya hapo akiwa mjini Kinshasa mpatanishi huyo maalumu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alitaka kuheshimiwa kwa serikali halali ya nchi hiyo, katiba yake, pamoja na mamlaka yake.

"Tunayo serikali iliyochaguliwa ambayo uhalali wake lazima tuulinde. Pili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina katiba ambayo lazima iheshimiwe na hatimaye, kuheshimiwa kwa mamlaka ya eneo la Congo, alisisitiza Rais huyo wa zamani wa Kenya.  Ziara ya Uhuru Kenyatta katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni hatua ya karibuni katika mfululizo wa juhudi za kupunguza mzozo mashariki mwa nchi hiyo.

Rais huyo wa zamani aliwasili katika mji mkuu wa Congo wa Kinshasa siku ya Jumapili kwa mazungumzo na wakuu wa serikali kufuatia ziara ya Rais wa Angola Joao Lourenco.

342/