Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

12 Februari 2024

19:23:33
1437178

Zaidi ya wanajeshi 11 wa Israel wauawa katika "shambulio kubwa" huko Khan Yunis

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba, jeshi la utawala huo ghasibu limekabiliwa na shambulio kubwa na la kushtukiza la wapiganaji wa Wapalestina huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambalo limeua zaidi ya wanajeshi 11 wa utawala huo.

Mamlaka ya Utangazaji ya Israel imesema kuwa jeshi la utawala huo "linakabiliwa na hali ngumu huko Khan Yunis baada ya shambulizi kubwa la kuvizia la wapiganaji wa Kipalestina, huku mapigano yakiendelea kati ya Muqawama na vikosi vya utawala uvamizi katika Ukanda wa Gaza.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa "tukio kubwa la usalama ni shambulio la kuvizia dhidi ya jeshi la Israel kusini mwa Khan Yunis," ikibainisha kuwa "jeshi la Israel litatoa maelezo kuhusu kile kilichotokea Khan Yunis saa chache baadaye."

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kuwa: "Tukio hilo limejiri kusini-mashariki mwa Khan Yunis kwa njia ya shambulio kubwa la kushtukiza na kwamba ilichukua masaa kadhaa kusafirisha maiti na majeruhi." 

Itakumbukwa pia kuwa kikosi cha Al-Qassam - tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) - kilifanya operesheni ya aina yake mnamo Januari 22 katika kambi ya Al-Maghazi katikati mwa Ukanda wa Gaza, ambapo maafisa na wanajeshi 21 wa Israeli walikuwa. 

342/