Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

23 Februari 2024

16:28:00
1439818

Haj Ali Akbari: Uchaguzi ni fursa nzuri kwa watu wa Iran

Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa iliyosaliiwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, uchaguzi ni fursa nzuri kwa watu wa Iran.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa wiki ijayo.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran amebainisha kwamba, uchaguzi ni nembo ya uhuru na mfumo wa dini nchini Iran wenye ridhaa ya wananchi.

Uchaguzi wa 12 wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi wa sita wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu utafanyika tarehe Mosi ya mwezi ujao wa Machi.

Sheikh Haj Ali Akbari ameashiria pia kuhusu kadhia ya kwanza ya ulimwengu wa Kiislamu na kimataifa  yaani Gaza na kkuibainisha kwamba, baada ya siku 140, vita vya Gaza vimekuwa dhihirisho kubwa la kushindwa kwa njia tofauti ubeberu wa kimataifa. Amesema, utawala ghasibu wa Kizayuni umepata pigo kubwa kutoka kwa wanamapambano wa muqawama na kwa msaada wa Mungu na juhudi za muqawama sambamba na mwamko wa kimataifa uliotokea, utawala huu katu hautaona siku nzuri.

Kadhalika khatibu wa Swala ya Ijumaa amesema, mauaji na uharibifu wa miundo mbinu huko Palestina na Gaza ni zao la demokrasia ya kkiliberalio ya nchi za Magharibi na kimya cha usaliti wa baadhi ya serikali zinazojiita za Kiislamu.

342/