12 Januari 2025 - 18:11
Kughairi mpango wa ISIS wa kulipua Haram Tukufu la Hazrat Zainab (s.a)

Vyombo vya kijasusi vya Serikali mpya ya Syria vilidai kukwamisha mpango wa ISIS wa kulipua Madhabahu (Haram) ya Hazrat Zainab (s.a).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Chanzo katika Kitengo cha kijasusi cha Serikali Mpya ya Syria kilidai kuwa kimezuia mpango wa ISIS wa kulipua Madhabahu (Haram) ya Hazrat Zainab (s.a) katika viunga vya Kusini mwa Damascus, Mji Mkuu wa Syria.

Shirika rasmi la habari la Syria lilichapisha habari hii na kuandika: Chanzo hiki kilisema kuwa katika operesheni hii, watu waliokuwa wakijaribu kutekeleza kitendo hiki kikubwa cha uhalifu kuwalenga watu wa Syria walitiwa mbaroni.